Overview
Dream Big Microfinance (T) Limited inajishughulisha na utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo Tanzania Bara kwa ajili ya kukuza mitaji ya kuendeleza biashara zao. Imepata kibali namba MSP2-0319 kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuendesha biashara ya kutoa mikopo midogo ikifuata sheria ya Microfinance ya mwaka 2018 pamoja na kanuni zake za mwaka 2019.