​Mfumo wa Tausi ni jukwaa la mtandaoni lililoanzishwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) linalowezesha wananchi kununua viwanja vya serikali kwa urahisi, popote walipo. Ili kununua kiwanja kupitia mfumo huu, unatakiwa kuwa na mahitaji machache ambayo tutaenda kuongelea kwenye makala hii.

enter image description here

Jinsi ya Kujisajili na Mfumo wa Tausi Portal

​​Mfumo wa Tausi ni jukwaa la mtandaoni linalowezesha wananchi na wafanyabiashara kupata huduma mbalimbali za serikali, ikiwemo maombi ya leseni za biashara, uombaji wa vibali na leseni mbalimbali, pamoja na huduma nyingine ikiwa pamoja na huduma ya kununua viwanja. Ili kujisajili kwenye Mfumo wa Tausi, tafadhali fuata hatua zifuatazo:​

Kulingana na matumizi unaweza kuhitajika kuwa na mahitaji mengine ya ziada, lakini kwa upande wa mnunuzi wa Viwanja unahitaji nyaraka zifuatazo.

  • Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kutoka NIDA.
  • Namba ya simu iliyosajiliwa kwa kutumia Kitambulisho cha NIDA.
  • Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) ya binafsi kutoka TRA.​
  • Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi ya kampuni (Company TIN) kutoka TRA (ikiwa ni kampuni).​

Hatua za Kujisajili

Tembelea tovuti ya Tausi Portal, kisha moja kwa moja bofya sehemu ya "Create Account" baada ya kubofya sehemu hii utaletewa jedwali lenye njia mbili kuu za kuweza kujiunga.

  • Njia ya Kwanza ni "Question" - ambayo hii unatakiwa kujibu maswali sambamba na maswali yaliyo kwenye kitambulisho chako cha NIDA.
  • Njia ya Pili ni "One Time Password" - ambayo hii utatumiwa ujumbe mfupi wenye neno la siri la kutumia mara moja kwenye namba ambayo umesajili kwenye kitambulisho chako cha NIDA.

enter image description here

Njia zote mbili zinakuitaji kujua nyaraka zako zilizoko samamba na kitambulisho chako cha NIDA, Hivyo hakikisha unacho kitambulisho na taarifa zako kama mahitaji yalivyo orozeshwa hapo juu.

Jinsi ya Kutumia Tausi Portal Kununua Ardhi (Kiwanja)

Baada ya kufanikiwa kujisajili moja kwa moja, ingia kwenye mfumo kwa kubofya sehemu ya "Sign In", kisha andika namba yako ya NIN kicha andika password na endelea kwenye mfumo.

Baada ya kuingia kwenye mfumo bofya sehemu ya "Land Sales" iliyopo upande wa kushoto juu, kisha changua "My Application", kwa sababu bado hujafanya manunuzi yoyote utaona sehemu ya "No Application" na kitufe cha "Apply Now" kwa chini yake. Bofya hapo ili kuona miradi inayopatikana kwa muda huo.

enter image description here

Miradi inayopatikana itakuwa chini ya kipengele cha "Available" na Miradi ambayo imeshauzwa itapatikana kwenye sehemu ya "Sold Out". Bofya kwenye Available kisha chagua aina ya Mradi kulingana na sifa na mkoa au wiliya unayo hitaji.

enter image description here

Angalia Viwanja kwenye ramani kisha bofya sehemu ya kiwanja ulicho kipenda na soma maelezo ya sifa za kiwanja yanayotokea mara baada ya kubofya kiwanja ulicho chagua.

enter image description here

Kumbuka ramani inaonyesha rangi ya Kijani, Nyekundu na Njano zikiwa zina ashiria kuwa viwanja vyenye "Rangi ya kijani" bado vinapatikana, na viwanja vyenye "Rangi nyekundu" vimesha nunuliwa. Pia "Rangi ya njano" inaonyesha viwanja ambavyo viko kwenye hatua ya uangalizi.

enter image description here

Jinsi ya Kufanya Manunuzi

Kabla ya kufanya manunuzi ni muhimu kufahamu kuwa unatakiwa kusoma vigezo na masharti muhimu ambayo ndio yatakupa mwongozo wa jinsi ya kufanya malipo na kukamilisha manunuzi. Sheria hizo ni pamoja na

  • Muombaji atalazima kufanya maombi ya kiwanja kupitia Mfumo na kulipia kiasi cha Tshs. 20,000 (Kama ada ya Maombi)
  • Ulipaji wa Ada ya Maombi ya Kiwanja Tsh 20,0000/= utamwezesha muombaji kuchagua kiwanja na kupata Namba ya Malipo (Control Number) ya kiwanja alichochagua. Muombaji atakapochelewa kuchagua kiwanja hatapata fursa ya kurejeshewa fedha aliyolipia kwa ajili ya ada ya maombi.
  • Malipo ya Maombi ya Kiwanja Tsh 20,000/= yafanyike ndani ya siku saba (7), baada ya siku hizo kuisha kiwanja kilichochaguliwa kitarejea sokoni kuchaguliwa na muhitaji mwingine na hakutakuwa na taarifa zaidi kwa muombaji wa awali.
  • Kiwanja kilichochaguliwa kitatakiwa kulipiwa fedha za ununuzi asilimia Hamsini (50%) ndani ya Siku saba (7) tangu tarehe ya kukichagua, kiasi kilichobakia kilipwe ndani ya siku tisini (90). Kushindwa kulipia fedha zote za kiwanja husika ndani ya muda huo, kiwanja hicho kitarudi sokoni na kuchaguliwa na mwombaji mwingine. Fedha yote ya awali iliyolipwa na mwombaji wa awali kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kilichoochaguliwa haitarejeshwa na hakutakuwa na taarifa zaidi kwake.
  • Malipo yote yatafanyika kwa kutumia Namba ya Malipo (Control Number) ambayo muombaji ataipokea kwa njia ya mfumo wakati anafanya maombi ya kiwanja.
  • Maombi, Ada ya maombi pamoja na fedha za ununuzi wa kiwanja yatafanywa na muombaji/mnunuzi kwa kupitia Mfumo wa Tausi.
  • Ni sharti muombaji kuwa na namba ya Kitambulisho cha Uraia (NIDA) ili kuingia kwenye mfumo wa maombi na ulipiaji wa kiwanja (Tausi Portal).

Baada ya kusoma na kuelewa vigezo na masharti hayo basi unaweza kuendelea kwa kubofya sehemu ya Nunua au "Buy Now" na moja kwa moja unaweza kulipia ada ya maombi kisha na kuendelea na hatua zinazofuata.

enter image description here

Hitimisho

Na hizo ndio hatua za kununua kiwanja ama ardhi kupitia mfumo wa Tausi Portal, kumbuka ni muhimu kununua kiwanja kulingana na mahitaji ya mradi hivyo ni vizuri kusoma vigezo na sifa za maeneo kabla ya kununua ili kukidhi vigezo na masharti ya eneo husika.

Pia bei za viwanja hivi vya serikali ni rahisi zaidi ukilinganisha na bei nyingine hivyo watumiaji wengi hununua kwa hara na hivyo kuwepo miradi michache. Kama kwa namna yoyote umekosa kiwanja kupitia mfumo wa Tausi Portal unaweza kupata kiwanja kupitia Zoom Tanzania Marketplace.