Kwa watu wengi, kuitwa kwenye interview ya kazi ni kitu kikubwa.
Workopolis waliripoti kwamba 2% ya wagombea kazi ndio wanaitwa kufanya interview, tu. Kwa Tanzania, ambapo wastani ya maombi ya kazi ni 100, ina maanisha kwamba watu wawili tu ndio watakayoitwa kwenye interview.
Sasa, utapitaje hiki kizuizi ukiwa unatafuta kazi?
Jiandae. Jiandae. Jiandae!
Ukijikuta umebahatika kuitwa kwenye interview ya kazi, kuna baadhi ya hatua unayoweza kuchukua kujiandaa na interview hiyo ili kuongeza nafasi ya kupata kazi hiyo:
Fanya utafiti juu ya kampuni
Ni matumaini kwamba ulishafanya utafiti juu ya kampuni ulivyokuwa unaandaa CV na barua la kuomba kazi. Sasa, fanya utafiti zaidi kwa kutimia Google na mitandao ya kijamii na kuongea na ndugu, jamaa na marafiki wenye ujuzi na kampuni au sekta yake.
Nia ya kufanya utafiti huu ni kuelewa hiyo kampuni kwa kiundani zaidi, changamoto zake pamoja na kujua ni jinsi gani amabayo utaweza kuonyesha kwamba wewe utakuwa suluhisho ya baadhi ya matatizo yao. Kwa kifupi, unafanya utafiti ili wajue ni kwa nini wanakuhitaji.
Andaa mkakati wa kujibu maswali
Kuongea bila sababu au kutoa majibu yasiyo na maana hayatamfurahisha mwajiri wako. Badala yake, kuwa na mkakati wa kujibu maswali. Kwa mfano, ukiulizwa “Utatoa suluhisho gani kwa tatizo hii ya ______ kama ukipata kazi hii?”
Jibu lako linaweza likaanza kwa kusema “Kwenye kampuni yangu ya zamani, tulipata matatizo yaliyo fanana na hii”. Baada ya hapo, unaeleza ni hatua gani ulizochukua kupata suluhisho.
Mwisho, elezea matokeo ya hatua ulizochukua pamoja na ni nini ulichojifunza kitakachoweza kukusaidia kwenye kazi hii unayogombea.
Jibu maswali kabla ya interview
Kwa kuwa utakuwa umeshafanya utafiti wa kutosha juu ya kampuni pamoja na kuandaa mikakati ya kujibu maswali, jiandae zaidi kwa kujibu maswali kumi yanayoulizwa zaidi kwenye interview. Andika majibu yako alafu fanya mazoezi ya kuyajibu.
Pia, jaribu kufikiria maswali mengine kuhusu sekta hiyo ambayo mwajiri anaweza akakuuliza. Pitia CV na barua lako la kuomba kazi kuangalia kama kuna maswali yoyote yanayoweza kujitokeza. Kwa mfano, kama unaomba kazi kwenye sekta ambayo ni tofauti na ulichosomea chuo kikuu, mwajiri anaweza akakuuliza kwa nini unafanya hivyo. Jiandae kutoa majibu ya ukweli na yenye maana.
Fanya mazoezi ya Interview
Mazoezi ya interview ni njia nzuri sana ya kujiandaa na kuandaa majibu yako. Chagua rafiki, ndugu, au mfanyakazi mwenzako wa kufanya naye mazoezi ya interview.
Hakikisha una fanya mazoezi ya kumtazama mwajiri na kutabasamu wakati wa interview. Pia, kumbuka kuwa mtulivu na makini wakati wa interview.
Vaa kwa kishindo
Huwa tunapata habari kwamba wagombea kazi wenye sifa za kufanya kazi vizuri wanakosa kazi kwa kuwa mavazi yao kwenye interview hayakufaa. Sasa, ili isikutokee, siku mbili kabla ya interview, mpigie afisa wa rasilimali watu ili ujue kanuni za mavazi ya kampuni hiyo.
Kwa kifupi, kwenye interview hakikisha unavaa kama vile umeshafanya kazi hapo ili kuwawezesha kuona kwamba unaweza ukafaa kufanya kazi hapo. Pamoja na hayo, hakikisha kwamba umechana nywele, umeweka vipodozi vya kawaida, hunuki n.k
Pata habari zaidi kuhusu jinsi ya kuvaa kwenye interview ya kazi, hapa.
Jua ofisi ilipo
Sisi watanzania tuna tabia mbaya ya kuchelewa. Kwenye swala la kuitwa kwenye interview ya kazi, hii haitakubalika kabisa.
Kwa kweli, ukiitwa kwenye interview inabidi usiwe mtanzania kabisa ikija kwenye swala la muda wa kufika. Wahi! Wahi! Wahi!
Njia rahisi ni kujua ofisi zilipo, kabla ya siku ya interview, ili uweze kujua utatumia njia gani na muda gani kufika mapema siku ya interview. Pia, hakikisha unawahi kuanza safari ya kuelekea kwenye interview alafu usisahau kuzingatia foleni, ajali, ukchelewaji wa daladala n.k
Lala mapema siku kabla ya interview
Lala mapema iliuamke bila uchovu wowote siku ya interview.
Fanya Mazoezi kuongeza ujiamini wako
Badala yakupanik dakika za mwisho kabla ya interview yako, fanya kitu kitakacho kuongezea ujiamini wako. Kwa mfano, sikilizo nyimbo inayokupa msisimko, soma maneno mazuri au mashairi yakukupa moyo n.k. Hata rukaruka kidogo. Ila, usitoke jasho!
Amini kwamba ulijitahidi kadri ya uwezo wako
Mwisho wa siku, ukipata hiyo kazi au ukiikosa, amini kwamba ulijitahidi kadri ya uwezo wako. Hakikisha kwamba umejifunza kitu kwenye mchakato mzima wa interview. Kama umekosa kazi hiyo, wasiliana na mwajiri aliyekufanyia interview na muombe akueleze interview yako iliendaje. Pia, usichukulie kama vile umetendwa vibaya. Badala yake, tumia matokeo hayo kukuhamasisha kuboresha ujuzi wako.
Eh heh, tumeyajuaje haya yote?
Zaidi ya kuwa tovuti inayoaminika na kutumika kuliko zote nchini kwenye kutangaza na kuomba kazi Tanzania, tumefanya interview nyingi kuwatafuta wafanyakazi bora wa kujiunga nasi.
Kama Bado unatafuta ajira unaweza kuomba moja ya kazi kupitia tovuti ya Zoom Tanzania Hapa.