![](https://www.zoomtanzania.net/wp-content/uploads/2025/01/download-7.jpeg)
Nafasi za Ufadhili wa Masomo Uturuki Scholarship Turkiye Burslari 2025/2026
Job Role Insights
-
Date posted
2025-01-11
-
Closing date
2025-01-11
-
Hiring location
Tanzania
-
Career level
Senior
-
Qualification
Doctorate (Ph.D.) Doctorate Degree Master’s Degree Undergraduate Degree
-
Quantity
10 person
-
Gender
both
Job Description
Ubalozi unapenda kuarifu kwamba Serikali ya Uturuki imetangaza fursa za ufadhili wa masomo kupitia Mpango Maalum wa Ufadhili wa Elimu unaojilikana kama Turkiye Burslari. Ufadhili huo ni kwa ajili ya Shahada ya Kwanza, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu katika mwaka wa masomo 2025/2026.
Ufadhili huo unajumuisha ada ya masomo, posho ya kujikimu kwa mwezi, bima ya afya, tiketi ya ndege, udahili wa chuo na usajili wa kozi (University and Program Placement), makazi na gharama ya kujifunza Lugha ya Kituruki kwa mwaka mmoja (Turkish Language Course).
Taarifa zaidi kuhusu ufadhili huo ikiwemo sifa na taratibu za uombaji zinapatikana kupitia Tovuti (turkiyeburslari.gov.tr). Maombi yote kuhusu ufadhili huo yatafanyika kupitia tovuti tajwa kuanzia tarehe 10 Januari 2025 na mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 20 Februari 2025.
Kwa kuzingatia umuhimu wa fursa hizi katika kuimarisha umahiri wa rasilimaliwatu nchini, Ubalozi unatoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi hizo kwa lengo la kuliletea Taifa letu maendeleo.
Interested in this job?
0 days left to apply
Share this opportunity
Help others find their dream job